Meneja wa msanii Diamond Platinumz Hamis Taletale Maarufu kama "Babu Tale" ameandaa Michuano ijulikanayo kwa jina la MAGUFULI CUP litakalo shirikisha Jumla ya timu 8 kutoka mkoa Dsm kwa ajili ya kuhamasisha ushirikiano na kuwakutanisha vijana
Akizungumza na waandishi habari jijini Dsm Muaandaji wa Mashindano hayo Hamis Taletale Maarufu kama Babu Tale amesema michuano hioyo inalenga kuwa kuwakutanisha vijana pamoja ili kujenga ushirikiano katika ufanyaji wa kazi.
Michuano hiyo itashirikisha timu za Friends
Rangers, Abajalo, Zakim, Toa Moyo, Burudani, Fc Kauzu, GombS united na
Faru Jeuri itaanza kutimua vumbi Oktobar 9 huku mshindi akindoka na kitita cha shilingi Milioni 5.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment