Jeshi la Polisi Kanda Maalum Jijini Dar es salaam linawashikilia watu Saba kwa tuhuma za ujambazi na Ugaidi wakiwa na silaha sita ambapo pia wanadaiwa kuhusika wa Uvamizi wa Vituo vya Polisi na Mauaji.
Aidha jeshi hilo pia limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa wengine sita ambao wanadaiwa kuhusika na mauaji ya Afisa wa Polisi ASP Elibariki Palangyo yaliyotokea nyumbani kwake Yombo Makangarawe August 4 mwaka huu.
Kamishna wa Polisi Kanda maaalum ya Dar es salaam,Cp Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari amesema Watuhumiwa hao wa ujambazi na Ugaidi wamekamatwa katika Operesheni maalumu inayoendelea katika jiji hilo kwa kushirikiana na mikoa jirani.
Amemtaja kiongozi wa kundi hilo la majambazi na kuendesha Vitendo vya Ugaidi kuwa Omar Saleh ambaye alikuwa na wenzake sita ambapo baada ya polisi kuvamia kambi yao na kuwatia mbaroni kiongozi huyo alijaribu kutoroka na kujeruhiwa kwa risasi na kufariki dunia.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment