REST IN PEACE MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA


Mwenyekiti wa chama cha siasa cha Democractic Party DP Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia jana alfajiri majira ya saa kumi na moja na dakika kadhaa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Msolwa wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani Jafari Mohammed, ambapo taarifa ya jeshi hilo imesema ajali hiyo imehusisha gari  aina ya toyota Corolla lenye namba T 183 AGM ambalo Mchungaji Mtikila akiwa na abiria wenzake watatu wakitokea Morogoro liliacha njia na kupinduka.

Taarifa hiyo imemtaja dereva wa gari hilo aliyenusurika kuwa Steven George Mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi

Mganga mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Tumbi iliyopo mjini Kibaha mkoani Pwani amethibitisha kupokea mwili wa marehemu mchungaji Christopher Mtikila pamoja na majeruhi wawili walioumia sehemu za kichwani ambapo amesema hali zao zinaendelea kuimarika.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment