Kada mkongwe wa Chama cha Mapinduzi, Kingunge Ngombale Mwiru, jana ametangaza rasmi kuachana na chama hicho kutokana na sababu kadhaa miongoni mwake ni kile alichodai uongozi wa CCM kubinafsisha chama na kufanya maamuzi wayatakayo pamoja na kushindwa kuheshimu katiba ya CCM.
Kingunge Ngombale Mwiru ambaye amedai kuwa ndani ya siasa ya Chama Tawala kwa zaidi ya miaka 61, amesema hana nia ya kujiunga na chama chochote cha Siasa, lakini anaunga mkono Mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, bw Edward Lowasa.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es salaam, Kingunge amesema anaunga mkono sera ya mabadiliko, kutokana na chama Tawala kuwa madarakani kwa muda mrefu sasa na kukieleza kuwa kimeishiwa pumzi na hakiwezi kuleta mabadiliko yanayotegemewa na watanzania wengi.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment