BAADA YA KUZISHUSHIA KICHAPO TIMU ZA MBEYA SASA MABINGWA YANGA KUWASILI JIJINI KUIKABILI AZAM FC

 

 

 

 Mabingwa Wa soka Tanzania Bara timu ya Yanga wanatarajiwa kurejea jijini Dar Salaam,kutoka mkoani Mbeya ambako iliweka kambi kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.


Yanga itarejea jijini na inatarajiwa kuingia kambini moja kwa moja kuendelea na mazoezi kabla ya mtanange wao na Azam FC iliyopo Visiwani Zanzibar ikijiwinda na mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya tanzania Bara,inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Semptemba 12.


Akizungumza na waandishi wa nhabari Afisa Habari wa Yanga Jerry Muro, amesema kuwa Yanga inaingia kambini ikiwa tayari imefanya vyema katika kichezo kadhaa ya kirafiki iliyocheza,ambayo imeonyesha mapungufu machache ambayo kocha wa Yanga anaendelea kuyafanyia kazi.


Aidha amesema kuwa kikosi hicho ambacho kimesheni nyota kadhaa mahiri kinaingia kambini kikiwea na lengo la kufanya vyema katika mchezo wake na Azam FC


Kwa upande mwingine Muro amesema kikosi hicho kinakabiliwa na baadhi ya wachezaji majeruhi akiwepo nahodha wa kikosi hicho ,Nadir Haroub 'Cannavaro' pamoja na mshambuliaji mahiri raia wa Burundi Hamis Tambwe na Oscar wote wakisumbuliwa na malaria .

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment