Baraza la sanaa taifa (BASATA) limetangaza kulifungulia shindano la urembo la Miss Tanzania baada ya waandaji wa mashindano kampuni ya Lino international agency kurekebisha baadhi ya kasoro zilizojitokeza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam katibu mtendaji wa baraza la sanaa taifa Geofrey Mngerteza amesema baraza limamua kuyafungulia mashindano hayo kufuatia waandaji kuomba radhi pamoja na kutekeleza baadhi ya kanuni na taratibu za uendeshaji wa mashinado hayo ikiwemo kukamilisha usajili wa mawakalam wa ngazi zote za mashindanio.
Aidha mngereza amesema kuwa baraza wametoa miezi minne ya uwangalizi kwa waaandaji wa mshindano hayo kushughulikia baadhi ya changamoto zalizosalia
Pia Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Lino international agency Hashimu Lundenga amesema kwa sasa kampuni hiyo imejapanga vya kutosha kuhakikisha inakabiliana na changamoto zilizojotokeza awali hazijiludii tena.
mashindano ya Miss tanzania yalifungiwa december 22 mwaka jana kufuatia kugubikwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo kwa aliyekuwa mshindi wa mashindani hayo SITTI MTEMVU
0 maoni:
Post a Comment