ENRIQUE AKIHOFIA KIKOSI CHAKE


                                           


                                       (Luis Enrique kocha mkuu wa barcelona ya hispania)

 

Kocha wa barcelona luis Enrique ameingia katika wasiwasi wakutetea mataji ya Uefa ligi kuu ya hispania pamoja na lile la kombe la mfalme kufuatia kikosi chake  kupokea kichapo cha bao 4-0 dhidi ya Athletico Bilbao katika mechi ya kombe la Super Cup.

Kocha huyo ambae alipata mafanikio mengi msimu uliopita kwa kunyakua mataji matano alikishuhudia kikosi chake kikichapwa mabao hayo kufuatia kuanzisha wachezaji wasiokuwa uzoefu na kupelekea mpaka wakati wa mapumziko ikiwa nyuma kwa goli 3-0.

kipindi cha pili kilianza kwa kocha luis Enrique kwa kufanya mabadiliko ya kuwaingiza baadhi ya nyota wake lakini mambo hayakubadilika baada ya mchezaji timu kuongezwa goli la 4 kupitia kwa mchezaji  Aritz Aduriz aliefumania  wavu mara tatu katiuka mechi hiyo.

Kikosi cha Enrique sasa kinakibarua kizito cha kubadilisha matokeo hayo ya mabao 4-0 ili kuweza kunyakua kombe hilo linaloashiria kufunguliwa kwa ligi kuu ya soka nchini hispania. 

 












Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment