Tanzania mpya itakayoundwa na serikali ya awamu ya tano itaboresha Sekta ya Kilimo kwa kuanzia upatikanaji wa pembejeo kwa wakati na za kutosha, ikiwa ni pamoja na mfumo wa soko la mazao.
Akiomba kura kwa wanaccm na wananchi wilaya ya Ludewa mgombea urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli amesema ataanza kupambamba na changamoto za sekta ya kilimo baada ya kuona baadhi ya pembejeo zinazotumika kwa ajili ya kupandia zinachelewa kuwafikia wakulima na zikifika hazitoshelezi mahitaji yao.
Kwa upande wake mjumbe wa kamati kuu ya CCM William Lukuvi akimwombea kura za urais Dk. Magufuli amewataka wananchi kuchagua chama chenye Sera nzuri zenye kutekelezeka cha CCM sambamba na uwezo wa utendaji kazi alionao Dk.Magufuli.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph
0 maoni:
Post a Comment