Kiongozi wa chama cha ACT-wazalendo Zito Kabwe ameliomba shirikisho la mpira Tanzania Tff kufuta kingilio kwenye mpambano wa timu taifa ya Tanzania dhidi ya Nigeria itakayofayika september 5 mwaka huu kwenye dimba la uwanja taifa jijini dsm.
Zito ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa ufunguzi wa kampeni wa chama hicho ambapo ameliomba shirikisho la soka Tanzania Tff kuwaruhusu watanzania kuingia bure kwenye mtanange wa taifa stars dhidi ya Super Eagles kwa ajili ya kufuzu michuano ya afcon.
Aidha kiongozi huyo wa ACT -wazalendo amewataka watangaza nia katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo urais , Ubunge , na udiwani kuunga mkono timu ya ya tafa ili iweze kufanikiwa kushiriki kwenye michuano ya kimatifa.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph
0 maoni:
Post a Comment