Serikali kupitia Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo imepiga marufuku Uzinduzi wa kampeni za Kisiasa zilizopangwa kufanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tarehe 22 mwezi huu katika Uwanja wa Taifa wa Michezo.
Akizungumza jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Asa Mwambene amesema kuwa Uwanja wa Taifa Utatumika kwa maswala ya michezo tu na sio maswala ya siasa hivyo Shughuli yoyote ya kisaisa haitaruhusiwa kuendeshwa ndani ya Uwanja huo.
Mwambene amesema kuwaSerikali ina lengo la kuweka Uwanja huo katika mazingira rafiki yatakayolenga maswala ya michezo zaidi hivyo kitendo cha Kuharibu utaratibu na kuruhusu shughuli za kisiasa kufanyika kwenye Uwanja huo ni kwenda kinyume na taratibu hizo.
Upigaji marufuku huo umekuja baada ya uvumi ulioenea katika baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu Chama cha siasa cha CHADEMA kupanga kufanya uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi katika Uwanja huo.
0 maoni:
Post a Comment