WALIMU 4400 KUTOLIPWA MADAI YAO NA SERIKALI

 
Zaidi ya walimu 4487 wamegundulika kuwa ni walimu hewa baada ya mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali kufanya uhakiki wa madai yao ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 19.6 ndicho kilichotakiwa kulipwa na baada ya uhakiki kiasi halali kilibainika ni Shilingi Bilioni 5.7 tu.
 
Hayo yamebanishwa jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wizara ya Fedha Dk.Servacius Likwelile akifafanua madai ya mwaka 2014 ambayo tayari yamelipwa kwa walimu huku akisema endapo kuna mwalimu yoyote atakuwa hajaridhishwa na uhakiki huo anaweza kufikisha tena malalamiko.
 
Miongoni mwa mambo yaliyofanya ongezeko hilo la fedha ni pamoja na baadhi ya walimu kudai fedha zaidi ya mara moja, wengine kudai kiasi kikubwa cha fedha ambacho si halali na wengine kujitokeza katika sehemu mbili mwalimu shule ya msingi na sekondari.


Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment