WAZEE WA KUBETI WALALAMIKIA MAKATO MAKUBWA YA KODI


Licha ya kuwa ni sanaa ya kubahatisha, michezo ya kubashiri matokeo michezoni nchini maarufu kama "kubeti" kadri siku zinavyokwenda imeoekana kuwa miongoni mwa michezo ambayo imekuwa ikiteka hisia na akili za wadau mbalimbali hata kufikia hatua ya kuitambua kama njia ya kujiingizia kipato hususani kipindi hiki ambapo michezo mbalimbali zinandelea duniani.

SANGUJ ilizunguka katika baadhi ya maeneo ya biashara za michezo ya kubashiri vilivopo jijini Dar es salaam na kuzungumza na wadau wa mchezo huo ambapo wamesema kuwa licha ya mchezo huo kuonekana kuwateka watu wengi hasa vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa, imekuwa ikiwasaaidia vijana hao kumudu gharama za maisha pindi wapato matokeo chanya ya bashiri zao.

Licha ya michezo hiyo kuonekana kuwaongezea kipato kwa kiasi kikubwa, vijana hao wameiomba jamii kuupokea utamaduni huo kwa mtazamo chanya kutokana na uwazi na ukweli unaoonekana, lakini pia wameziomba mamlaka husika kuwatengenezea mazingira bora ya kutumia njia hiyo kujiongezea kipato kwa kuweka kodi zisizokandamizi kwenye biashara hiyo.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment