MEYA KINONDONI;WASANII TUNGENI NYIMBO ZA KUHAMASISHA NA AMANI NA UTULIVU #UCHAGUZIMKUU-OCT25


Wasanii wa muziki nchini wamekumbushwa kutunga na kuimba nyimbo za kuhamasisha amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.

Hayo yamesemwa na meya wa manispaa ya kinondoni Yusuph Mwenda kwenye hafla ya uzinduzi wa Dar kavasha family club ambayo inashirikisha watu tofauti tofauti pamoja na wadau wa muziki wa dansi wa zamani wenye mahadhi ya lugha za kiswahili na lingala.

Aidha bwana Mwenda aliongeza kuwa, wanamuziki wengi nchini hasa wa kizazi kipya wamekuwa na kawaida ya kuimba nyimbo zenye maudhui mchanganyiko huku wakisahau kuwa amani ya nchi ndio msingi wa maendeleo ya sekta yoyote ikiwamo ya muziki pia.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment