KITIME;WASANII UFANYIENI KAZI USHAURI WA RAIS KIKWETE


Mwenyekiti wa mtandao wa wanamuziki John Kitime amewataka wasanii mbalimbali nchini kufanyia kazi ushauri wa rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kujiunga na mifuko ya bima ya afya ili kuepukana na fedheha  pindi wanapokumbwa na matatizo  mbalimbali.

Kitime ameyasema hayo jijini dsm ambapo ameongeza kuwa msanii yeyote nchini anasifa ya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo itawapa fursa ya kuchangia na kutibiwa wakati wowote wakiwa maeneo yoyote hapa nchini.

Kauli hiyo ya Kitime imefata siku chache baada ya rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt Kikwete kuwashauri wasanii wa kitanzania kujiunga na mifuko hiyo, wakati hafla ilyofanyika ukumbi wa mlimani city mwanzoni mwa mwezi August ya kumuaga kiongozi huyo

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment