TANESCO; MIKOA 16 IKIWEMO DODOMA, MWANZA, IRINGA, ARUSHA, DSM, TANGA, ZANZIBAR KUKOSA UMEME SIKU 7


Shirika la umeme Tanesco, leo linaanza rasmi uunganishaji wa gesi kwa ajili ya kufua umeme kwenye mitambo yake iliyopo Ubungo jijini Dar es salaam, hatua itakayosababisha mikoa zaidi ya 16 kukosa umeme kwa siku saba kuanzia leo.

Mikoa inayotarajiwa kukumbwa na tatizo la ukosefu wa umeme ni Dar es salaam, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Dodoma, Morogoro, Singida, Mwanza, Mara, Mbeya, Iringa, Tabora, Shinyanga, Manyara na Zanzibar.

Kutokana na hatua hiyo, watendaji wakuu wa Shirika la Umeme Tanzania na Shirika la Maendeleo ya Petroli wamewaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu utakaojitokeza wakati wa uunganishaji wa gesi kwenye mitambo ya kufua umeme na wamewahakikishia kuwa kukamilika kwa hatua hiyo kutalisaidia taifa kuwa na umeme wa Uhakika.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment