MADRID KUISHITAKI MAN U FIFA, KUKWAMA KWA USAJILI #DEGEA

De Gea's relationship with United boss Van Gaal is in tatters and the goalkeeper is said to be 'devastated'\

Klabu ya Real Madrid ya nchini hispania imetishia kuishitaki Manchester united katika bodi ya fifa inayohusika na maswala ya uhamisho wa kimataifa kufuatia kile wanachokidai united kuchelewesha karatasi muhimu za kukamilishausajili wa David Degea katika timu hiyo.

Madrid walifikia uamuzi huo muda mfupi baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili nchini hispania hapo jana, ambapo taarifa kutoka nchini humo zinasema kuwa Manchester United wamekwamisha dili la mlinda mlango huyo.

Kwa upande wao Manchester United wamesema kuwa wana vithibitisho vinavyoeleza wamefikisha karatasi hizo kwa wakati kwenye  chama cha soka cha nchini Hispania (SFF) kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili nchini humo.

Madrid walikua tayari kutoa dau la pauni milioni 29 ,pamoja na kipa wao Keylor Navas kama sehemu ya dili lauhamisho huo. pia Kusalia kwa De Gea katika timu hiyo anakuwamiongoni mwa makipa  wanne akiwemo Sergio Romero,Victor Valdezna kinda Sam Johnstone.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment