TADIP;LOWASA ATACHAGULIWA KWA 54% MAGUFULI 40%


Utafiti uliofanywa na Taasisi isiyokuwa ya kiserikali inayojishughulisha a masuala ya utafiti TADIP umeonesha kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chadema chini ya mwamvuli wa ukawa anaongoza kwa asilimia 54 kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu.

Kwa mujibu wa utafiti huo mgombea huyo wa urais kupitia CHADEMA ataibuka kinara kwenye uchaguzi mkuu kwa kuungwa mkono na makundi mbalimbali ya watu kutoka katika mikoa 10 ambayo imefanyiwa utafiti na taasisi hiyo, miongoni mwa mikoa hiyo ni  Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Dar es salaam

Mwenyekiti wa bodi ya TADIP George Shumbusho amesema kuwa mgombea huyo wa ukawa anakubalika kwa zaidi ya asilimian 54 akifuatiwa na mgombea wa CCM, Dk John Magufuli kwa asilimia 40 huku mgombea urais kwa tiketi ya chama cha ACT wazalendo Anna Mgwila akikubalika kwa asilimia 2.

Vilevile utafiti huo umeonyesha kuwa Chama cha Mapinduzi kinakubalika zaidi katika ngazi ya Ubunge kwa aslimia 40 wakati Chadema kikifuatia kwa asilimia 30 huku vyama vingine ACT ikiwa na  asilimia 3 CUF asilimia 2,  NCCR na TLP vikikubalika kwa asilimia 2 kila kimoja 

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment