Mabingwa wa ligi kuu soka uingereza timu ya chelsea the blues leo imeishushia kichapo cha goli 2-0 wapinzani wao wao jadin kutoka jiji la london timu ya arsenal katika mchezo wa mapema wa wa ligi hiyo uliofanyika kwenye dimba la stamford Bridge nchini uingereza.
Chelsea ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa beki wa kati Kourt Zouma kunako dakika ya 53 baada ya kupiga kichwa kikali kilichomshinda mlinda mlango wao wa zamani Petr Cech na kuifanya chelsea iongoze kwa goli 1-0 dhidi ya washika bunduki hao waliokuwa wakicheza wakiwa na wachezaji 9 uwanjani baada ya beki wake Gabriel Paulista na kiungo wake Santi Cazola kuoneshwa kadi nyekundu kunako dakika ya 45 na dakika ya 79.
Chelsea ilijihakikishia ushindi wake na kuondoka na pointi zote tatu kwenye dimba lake nyumbani baada ya kupata goli lake la 2 kunako dakika ya 90 za kipindi cha pili kupitia kwa mchezaji mahili Eden Harzad baada ya kupokea pasi maridadi kutoka kwa Oscar.
Mpaka mwisho wa mchezo huo chelsea ilitoka kifua mbele kwa kupata jumla ya pointi tatu na hazina ya mabao mawili huku ikisogea hadi kwenye nafasi ya 13 ya msimamo waligi hiyo inmyoongozwa na Manchster city wenye alama 15.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment