Bingwa wa WBC NA WBA Floyd Mayweather ametangaza kustaafu tasnia ya masumbwi duniani baada ya kushinda pambano lake la 49 dhidi ya bondia mwenzake wa marekani Andro Berto kwenye pambano la raundi 12 lililofanyika katika ukumbi MGM las Vegas nchini Marekani.
Mmarekani huyo mwenye miaka 38 amefikia uamuzi huo baada ya kumpiga Andre Berto kwa alama 120-108, 118-110 na 117-111 huku akitumia staili yake ya kujilinda kama alivofanya wakati wa pambano lake la may 2 mwaka huu dhidi ya mfilipino Manny Pacquao.
Amesisitiza kuwa hilo litakuwa pambano lake la mwisho na kwa sasa atajikita zaidi katika kuangalia familia yake, wakati akiwa amefikia rekodi ya bondia wa zamani wa martekani Rocky Marciano aliyecheza mapambano 49 bila kupoteza.
Mayweather amecheza jumla ya mapambano 49 tangu alipoanza kushiriki michezo hiyo mwaka 1996 alipocheza dhidi ya mmexiko Roberto Apodaca na kushinda jumla ya mapambano 26 kwa KO
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment