Shirikisho la mpira wa miguu duniani Fifa limemsimaisha katibu mkuu wake Jerome Valcke kutokana kile kilichodaiwa kuwa katibu huyo amehusika katika ubadhilifu wa fedha na uchukuaji rushwa katika utendaji wake wa kazi.
Taarifa zinaeleza kuwa miongoni mwa makosa ya kiongozi huyo ni kuongeza gharama za kununulia tiketi wakati wa kombe la dunia 2014 nchini brazili, ikiwa ni asilimia 17 zaidi ya gharama zilizoainishwa ili kujipatia fedha isivyo halali.
Pia kwa mujibu taarifa za ndani kutoka shirikisho hilo kupitia kwenye mtandao wake zinasema kiongozi huyo wa ngazi ya juu amekiuka kanuni na sheria ya uuzaji wa tiketi zilizowekwa na shirkisho hilo hivo amesimamishwa kushika wadhifa wake mpaka kamati ya maadili ya shirikisho hilo itakapokamilisha uchunguzi wa tuhuma hizo.
Jerome Valcke anatuhumiwa pia na sakata la kupokea dola za kimarekani milioni kumi ili kutoa nafasi ya mashindano kombe la dunia mwaka 2010 kwa taifa la Afrika Kusini jamba ambalo yeye amekanusha kuhusika.
Tuhuma hizo kwa Valcke mwenye miaka 54 zinaenda sambamba na zile zilitokea mwezi may mwaka huu ziliohusisha maafisa wa shirikisho hilo wakihusika katika utakatishaji pesa pamoja
na matumizi mabaya ya fedha
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment