Vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi - Ukawa, vimeelezea kusikitishwa na kile ilichokieleza kuwa vitendo vya hujuma wanavyofanyiwa na wale waliowaita wapinzani wao kisiasa.
Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa ukawa ambae pia ni mwenyekiti wa Taifa wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, amesema miongoni mwa hujuma umoja huo unaofanyiwa ni kuchaniwa mabango ya wagombea wa vyama hivyo kwa ngazi ya Ubunge na Urais, na kueleza kuwa baadhi ya vijana wamekuwa wakivaklishwa nguo za vyama vinavyounda umoja huo na vijana hao kutumiwa kwa lengo la kufanya vurugu,
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam, Bw James Mbatia amezitaka mamlaka zinazohusika kuanzia vyombo vya dola na Tume ya taifa ya Uchaguzi kuchukua hatua mapema ili kudhibiti hali hiyo ambayo ameielezea kuwa huenda ikasababisha uvunjifu wa amani.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph
0 maoni:
Post a Comment