Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA anayewakilisha umoja wa vyama vinne vya upinzani vinavyounda UKAWA Edward Lowassa leo amefanya ziara ya kushtukiza katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ili kujionea kero zinawakabili wakazi wa jiji hilo ikiwemo adha ya usafiri na mazingira magumu ya wafanyabiashara wa chakula maarufu kama mama lishe.
Akiwa ameongozana na mgombea mweza Juma Haji Duni mapema asubuhi wanawasili eneo la kituo cha daladala cha gongo la mboto ili kujionea hali halisi ya adha ya usafiri inayowakabili wakazi wa jiji hilo .
Mgombea urais huyo kwa tiketi ya CHADEMA anadiriki kuungana na wakazi wa dar es salaam kupanda daladala kutoka kituo cha Gongolamboto mpaka Chanika, (ili) na baadhi ya abiria wakitumia mwanya huo kumueleza kero zinazowakabili katika kazi zao za kila siku.
0 maoni:
Post a Comment