Kampuni ya Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro kimetoa udhamini wa vifaa mbalimbali venye thamani ya sh milioni 70 kwa timu za simba na Yanga kwa ajili maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Akikabidhi jezi, mipira, soksi pamoja na vifaa vingine vya michezo mbele ya waandishi wa habari jijini dar es salaam meneja bidhaa wa bia ya kilimanjaro Pamela Kikuli amesema hiyo ni sehemu ya hatua kwa kampuni hiyo katika kuhakikisha inakuza na kuendeleza soka la tanzania.
kwa upande wao mkuu wa idara ya masoko wa Yanga Omari Kaya pamoja na Collin Friech ambae ni kaimu katibu mkuu wa Simba sports Club wameishukuru bia ya kilimanjaro kwa udhamini huo huku wakitoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini ili kuleta mvuto zaidi kwenye ligi hiyo.
Meneja Bidhaa k/njaro akiwakibidhi vifaa afisa masoko yanga Omari Kaya (kushoto) Collin Friech kaimu katibu simba (kulia) |
Meneja Bidhaa k/njaro akiwakibidhi vifaa afisa masoko yanga Omari Kaya (kushoto) Collin Friech kaimu katibu simba (kulia) |
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph
0 maoni:
Post a Comment