Kikosi cha wachezaji 18 kinachounda timu ya soka ya taifa wanawake Twiga Stars kinaondoka nchini september 1 kuelekea CongoBrazaville kushiriki michuano ya all Afrika game inayoanza kurindima mapema wiki hii.
Akizungumza na SANGUJ jijini dar es salaam kocha mkuu wa Twiga stars Rogasian Kaijage amesema kuwa timu iko tayari kwa ajili ya mashindano hayo na kupitia kikosi hicho atafanya vizuri kwenye michuano hiyo.
Aidha Kaijage ameongeza licha ya kuwepo kwa ugumu katika kundi lake linalohushisha timu za ivory Cost , Congobrazaville pamoja na Nigeria anaamini mchezo wa soka hauna mwenyewe hivo timu yoyote inaweza kupata nafasi ya kusonga mbele.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph
0 maoni:
Post a Comment