Timu ya taifa kwa Mchezo wa ngumi inatarajia kuondoka nchini august 28 kuelekea Congo barazaville kwa ajili ya kushiriki kwenye michuano ya all afrika game itakayoanza kurindima September 5 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi habari leo Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama cha mchezo wa ngumi Tanzania Bft , Makore Mashaga amesema kuwa timu hiyo itawakilishwa na mabondia watatu waliopatikana kwenye orodha ya wachezaji 17 ambao walikuwa wakifanya mazoezi kwenye uwanja wa ndani wa taifa.
Aidha Mashaga ameongeza kuwa kutokana na mafunzo waliyopata wachezaji hao kutoka kwa kocha mkuu wa timu hiyo anaamini kikosi hicho kitaipeperusha bendera ya nchi kwa kurudi na medali mbalimbali,
0 maoni:
Post a Comment