Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi ya wiki iliyopita nchini Burkina Faso Jenerali Gilbert Diendere hii leo alitarajiwa kukabidhi madaraka kwa rais aliyempindua,
Michel Kafando baada ya shinikizo kubwa kutoka viongozi wa kikanda. Makubaliano yamefikiwa kati ya jenerali huyo na jeshi la nchi yake usiku wa leo, hii ikiwa ni kwa mujibu wa wawakilishi wa pande hizo mbili.
Makubaliano hayo yamejengwa juu ya vipengele vitano, ambavyo vinajumuisha kile kinachowataka wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa rais kilichojaribu kufanya mapinduzi - RSP, kurejea katika kambi yao, na kuondoka katika vituo walivyovikamata katika mji mkuu wa nchi, Ouagadougou.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment