FAHAMU DHUMUNI LA SAFARIN POPE FRANCIS NCHINI MAREKANI

 
Rais Barack Obama wa Marekani  kwa mara ya kwanza amemkaribisha kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, katika ikulu ya nchi hiyo, hii leo.

Mizinga 21 ilipigwa kwa heshima ya  kiongozi huyo wa kanisa katoliki, kama ishara ya kumkaribisha mtu anayechukuliwa kuwa na nguvu za kimaadili na mshirika wa kisiasa kwa Obama. 

Awali Rais Obama mwenyewe alikwenda uwanja wa ndege kumpokea Papa Francis, akiwa akiwa na Makamu wake wa Rais Joe Biden pamoja na  familia ya Obama.

Mkutano huu unaashiria maelewano baina ya viongozi hao wawili juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, kukosekana kwa usawa, mgogo wa wahamiaji, pamoja na kurejeshwa mahusiano baina ya Marekani na Cuba ambapo kabla ya kuwasili Papa Francis nchini Marekani pia alitembelea kisiwa cha Cuba.
 
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo 
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment