Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amewaonya matapeli wa viwanja na wavamizi wa ardhi ambao wamekuwa wakishirikiana na watendaji wa Halmashauri na Wizara ya Ardhi kuwapora ardhi wananchi ambao wana hati halali za kumiliki maeneo hayo.
Waziri Lukuvi ametoa onyo hilo leo jijini Dar es saalam baada ya kusikiliza kero mbalimbali na malalamiko ya wananchi wa wilaya za Ilala na Temeke kuhusu migogoro ya ardhi ambapo amesema Serikali imedhamiria kumaliza migogoro ya ardhi nchini.
Amesisitiza kwamba wale watakaobainika kuwadhulumu ardhi wananchi wanyonge, watavunjiwa nyumba walizojenga kwenye ardhi husika ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment