NEC;MWANANCHI ULIPOJIANDIKISHA NDIPO UTAKAPOPIGIA KURA


 
Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC imesema mwananchi yeyote ambaye amejiandikisha na kupata kadi halali ya mpiga kura, atakuwa huru kupiga kura kwenye kituo alichojiandisha na kuwa na haki ya kuchagua viongozi wanaoomba ridhaa ya kuchaguliwa kwenye eneo alilojiandikishia.
 
Ufafanuzi huo umetolewa na mkurugenzi wa Uchaguzi, Bw Ramadhan Kailima, wakati akizungumza na channel ten kwenye mahojiano maalum juu ya wasi wasi walio nao baadhi ya wananchi kuwa waliojiandikisha kwenye maeneo ambayo sio makazi yao hawataruhusiwa kupiga kura kwenye uchaguzi wa oktoba kutokana na kutokuwa wakazi wa maeneo hayo.
 
Katika hatua nyingine Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema ni kosa kwa watu wanaowalaghai wananchi kwa kununua kadi za kupigia kura na kueleza kitendo hicho ni kosa kisheria kwa anaeuza au anae nunua Kadi hiyo, Ambapo adhabu yake ni faini ya shilingi laki tatu au kifungo cha miaka mitatu gerezani au vyote kwa pamoja.


Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment