Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) umempitisha Sheikh Abubakar Zubeir kuwa Mufti (Sheikh Mkuu) wa Tanzania.
Sheikh Zubeir amepitishwa kuwa mufti katika uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma na kukosa mpinzani, baada Sheikh Ali Mkoyogole kujitoa katika dakika za mwisho katika uchaguzi huo, ambapo mufti huyo mpya alichukua wasaa huo kuwaomba waislamu wenzake kuliombea taifa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Uchaguzi wa Mufti wa Tanzania, umekuja baada ya aliyekuwa mufti wa hawali Sheik Shaaban Bin Simba kufariki dunia.
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment