MEMBE;WAANGALIZI WA KIMATAIFA HAMPASWI KUINGILIA UCHAGUZI WA TZ #UCHAGUZIMKUUOCT25


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa bwana Bernard Membe  amewataka waangalizi wa Kimataifa wanaokuja nchini kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba mwaka huu, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za Tanzania.

Bwana Bernard Membe ametoa angalizo hilo jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa akizungumza na mabalozi wote wanaoziwakilisha nchi zao na Mashirika ya Kimataifa nchini Tanzania, kuhusu uchaguzi mkuu huo ambao dalili zinaonyesha kwamba utakuwa na ushindani mkali.

Aidha, Waziri huyo wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa amesisitiza kwamba waangalizi hao wa Kimataifa hawapaswi kuingilia kwa namna yoyote mchakato wa uchaguzi, ikiwemo kutoa matamko na kuzungumza na vyombo vya habari kabla ya matokeo rasmi ya uchaguzi yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment