Kampuni ya vingamuzi ya star time imeingia makubaliano ya miaka 3 na shirikisho la mpira wa miguu tanzania tff yenye thamani ya shilingi millioni 900 kwa ajili ya udhamini wa ligi daraja la kwanza iliyoanza kutimua vumbi mwishoni mwa juma lililopita.
Akizungumza mbele tya waandishi habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Star Times Media LanFang Liao amesema kuwa mchezo wa soka umekuwa ukiongezeka kasi nchini Tanzania ukilinganisha na nchi nyingine za afrika mashariki kutokakna na kuwepo kwa hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa mchezo huo
Kwa upande wake rais wa shirikisho la mpira wa miguu tanzania Tff Jamal Mlainzi ameishukuru kampuni ya star times kwa udhamini huo huku pamoja na kutoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini kwa ;engo la kuinua soka la Tanzania
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph and +255712861292 kwa matangazo
0 maoni:
Post a Comment