ZAIDI YA WATU 107 WAFARIKI DUNIA KATIKA MJI MTAKATIFU WA MECCA SAUDIARABIA



Takriban watu 107 wamefariki dunia kufuatia kuanguka kwa WINCHI ya shughuli za ujenzi katika msikiti mkuu wa mji mtakatifu wa Mecca nchini Saudi Arabia kutokana na dhoruba kubwa iliyoambatana na mvua na upepo mkali hapo jana.

Taarifa zinasema idadi ya watu waliokuwa wamejeruhiwa katika tukio hilo ilikuwa imefikia 238, ambapo Serikali ya nchi hiyo haikuweza kuthibitisha mara moja utaifa wa watu waliopoteza maisha katika tukio hilo lakini  ni dhahiri kuwa vifo hivyo vinagusa mahujaji toka mataifa mbalimbali ambao walikuwa wameanza kuwasili Makka kwa ajili ibada ya Hija inayoanza baadae mwezi huu.

Ajali hiyo imetokea wakati wa mvua kubwa pamoja na upepo mkali uliosababisha ajali hiyo huku kukiwa kunafanywa maandalizi ya kuanza kwa ibada za Hijja.

Kufuatia ajali hiyo gavana katika eneo la Makka ameamrisha kufanyika uchunguzi kufuatia kuanguka kwa kreni katika msikiti huo mkubwa zaidi duniani.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment