YANGA IMELIPA MILIONI 31 KWA SHIRIKISHO LA SOKA #TFF KWA AJILI YA "MAPRO WAKE"


Klabu ya soka ya Yanga  ya jijini Dsm imesema imejiandaa vya kutosha kuhakikisha inatetea ubingwa wake wa ligi kuu soka Tanzania bara kutokana na klabu hiyo kukamilisha baadhi ya taratibu katika shirikisho la mpira wa miguu Tanzania tff

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es salaam afisa habari wa timu ya yanga Jerry Muro amesema kuwa kuelekea maandalizi ya ligi kuu soka tanzania bara iliyoanza kutimua vumbi leo klabu hiyo imelipa kiasi cha shilingi millioni 31 kwa ajili yavkukamilisha baadhi ya taratibu katika shirikisho hilo ikiwemo ulipaji wa dolla 2000 pamoja na kulipian kibari cha kufanyia kazi kwa  wachezaji wa kigeni

Akizungumizia kuhusiana na mpambano wa kesho dhidi ya Costal Union ya Tanga katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Mullo amesema kuwa timu hiyo itamkosa mchezaji Juma Abdul anaetumikia adhabu ya kuoneshwa kadi nyekundu alioipata kwenye mchezo wa mwisho wa timu hiyo.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment