NEC;UCHAGUZI UTAKUWA WA HURU NA HAKI, HAKUNA KURA ZITAKAZO IBIWA


Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imewahakikishia wananchi pamoja na vyama vya siasa nchini kuwa Uchaguzi unaotarajia kufanyika October 25 mwaka huu utakuwa huru na haki na hakuna wizi wa kura

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza katika mkutano na wenyeviti na viongozi wa tume za Uchaguzi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki na kati amesema Tume hiyo itahakikisha kuwa inasimamia haki na Sheria wakati wa uchaguzi na kumtangaza mshindi.

Aidha amesema kutokana na changomoto tume hizo zimekuwa zikilalamikiwa na wananchi hususan wakati wa Uandikishaji au Ukusanyaji wa matokeo Jaji Lubuva amesema kuwa tume ya tanzania imejitahidi kwa kiasi chake ili kukabiliana na changamoto hizo


 
Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo

Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment