TCRA YAWAKAMATA WAWILI KWA KUVUNJA SHERIA YA MTANDAO; WADAIWA KUBUNI AKAUNTI FEKI ZA RAIS KIKWETE. ZITO KABWE


Watu wawili wanaodaiwa kuwa Vinara wa kutengeneza Tovuti Bandia kwa kutumia Majina ya Viongozi mbali mbali ikiwamo jina Rais Kikwete mamlaka ya mawasiliano TCRA na kujipatia fedha kinyume cha Sheria wamefikishwa katika mahakama ya kisutu jijini dsm.

Washtakiwa hao Maximilian Rafael Msaki na Patrick James Natala wameshitakiwa kwa makosa kumi yakiwemo kutengeneza tovati kwa majina ya Jakaya Kikwete Foundation,Tcra Foundation ,Ridhiwani Social Company,Kampuni ya jamii ya mikopo ,Hisa Tanzania ,Akiba Saccoss, na Zitto Kabwe Foundation ambazo wahusika walikuwa wakizitumia kujipatia fedha kuanzia mwaka 2010 hadi 2015.

Mwendesha mashataka wa serikali amesema watuhumiwa hao pia walisajili simu kwa mitandao ya tigo,voda,airtel ambayo wamekuwa wakipokea Pesa kutoka kwa watu mbali mbali baada ya kuwaahidi kuwapatia mikopo kutoka katika taasisi hizo za kitapeli walizobuni.

Usipitwe..Jiunge nami kupitia Facebook ,Twitter , Instagram , Youtube, kwa jina la +Sangu Joseph  and +255712861292 kwa matangazo  
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment